Mkazo wa upatikanaji wa chakula shuleni unahitajika kupitia hamasa mbalimbali ili watoto waweze kusoma katika mazingira mazuri. Taarifa imesomwa Leo 12 Agosti,2025 katika kikao cha Tathimini ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mikataba ya afua za Lishe kwenye ukumbi mdogo wa Halmashauri.
Lengo la kikao ilikuwa ni kupima hatua zilizofikiwa katika uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa Lishe wanafunzi kupitia michango ya wananchi na imebainika imeongezeka kutoka asilimia 31 hadi kufikia asilimia 51 kwa robo ya nne ya mwaka 2024/2025.
Akizungumza katika kikao Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Mathamani amepongeza juhudu za kuhakikisha hali ya upatikanaji wa chakula shuleni imeongezeka kulingana na hapo awali kwa kutumia mbinu mbalimbali, hivyo amewataka watendaji wa Kata kufanya hesabu ya kuongeza hali ya upatikanaji wa Lishe mashuleni kwa kuwahamasisha wazazi ili kupunguza changamoto za Lishe Wilayani.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Uvinza Ndg James Mkumbo amesema mkazo wa Elimu ya Lishe uendelee kutolewa kupitia hamasa mbalimbali kwa jamii ili kuweza kutambua umuhimu wa afua za Lishe kwa watoto wanapokuwa shuleni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza CPA Fred Milanzi amesisitiza Elimu iongezeke kupitia vigezo vya upimaji kwa jamii kuongeza uelewa kwa jamii kuchangia chakula shuleni, ikiwa malengo ni kuondoa hali ya kuwa katika hatua hatarishi ya utapiamlo ukizingatia ni Wilaya yenye chakula cha kutosha.
Vilevile Afisa Lishe Wilaya ya Uvinza Ndg. Dismas Pokela amewataka watendaji wa Kata kuongeza ubunifu katika kuhamasisha afua za Lishe ili kuhimiza wanaume kushiriki.
District Executive Director (DED)
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0713518891
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.