Walimu wakuu 10 kutoka Shule zenye vituo vya MEMKWA na walimu 20 kutoka Shule za MEMKWA wamepatiwa mafunzo kazini yatakayo wajengea uwezo wa kuweza kufanya kazi kwa weledi, mafunzo hayo ni ya namna ya kutengeneza dhana zitakazo wawezesha kusaidia katika ufundishaji wa wanafunzi wa MEMKWA katika Shule zao.
Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku tatu mfululizo katika ukumbi wa Veta Wilayani Uvinza yakishirikisha Walimu Wakuu na walimu wa madarasa kutoka Shule zenye wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) kwa ufadhili wa Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ina vituo 24 vya MEMKWA, ambapo vituo 20 vinafadhiriwa na UNICEF na vituo 4 ni kwa ufadhili wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza. Hivyo wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) una lengo la kuwawezesha watoto wenye umri wa Miaka 9 Hadi 13 kupata Elimu stahiki.
District Executive Director (DED)
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0713518891
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.