Wakinamama wanaonyenyesha na wajawazito wa Kata ya Basanza wajitokeze katika kuadhimisha kilele cha wiki ya Unyonyeshaji wa maziwa ya Mama Duniani iliyoanza tarehe 1 hadi tarehe 7 Agosti,2025 yenye kauli mbiu "Thamini Unyonyeshaji, weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"
Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Unyonyeshaji yamehitimishwa katika zahanati ya Basanza Kata ya Basanza Wilayani Uvinza Leo tarehe 11 Agosti,2025. Wakinamama wanaonyenyesha na wajawazito kuzingatia umuhimu wa kunyonyesha kwani maziwa ya mama yanakinga ya kumlinda mtoto dhidi ya magonjwa.
Akihitimisha maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh Dinah Mathamani amesema Serikali kwa kuona Unyonyeshaji ni swala mtambuka inaweka nguvu na Mkazi kwa mama anayenyonyesha na jamii kwa ujumla ili kutambua umuhimu wa maziwa ya mama kwa kumjenga mtoto kiakili, kiafya na kisaikolojia ili mtoto aweze kukuza katika Msingi inayofaa.
Mh. Dinah ametoa rai kwa wanaume kutoa ushirikiano wa wenza wao wanapokuwa wajawazito kwenda kuhudhuria kliniki ili kujenga misingi imara kwa makuzi ya mimba mpaka pale mtoto atakapozaliwa na kuweza kunyesheshwa kikamilifu.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dr. Maira Biseko amewataka wakina mama wajawazito na wanaonyenyesha kuzingatia maelekezo na elimu ya Unyonyeshaji inayotolewa kliniki mara kwa mara ili kuweza kusaidia maendeleo ya makuzi mazuri ya mtoto.
District Executive Director (DED)
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0713518891
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.