IDARA YA MAJI
Idara ya maji ni moja kati ya Idara 12 za Halmashauri ya Uvinza na ilianzishwa rasmi tangu Julai, 2013 mara baada ya Halmashauri ya Uvinza kuanza. Idara ya Maji kwa sasa ina watumishi wa kuajiriwa wapatao 10.
MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Maji ikiwa ni moja ya Idara chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya inajishughulisha na kumsaidia/kumshauri Mkurugenzi Mtendaji Wilaya katika mambo yafuatayo:-
Kuandaa mipango na bajeti ya utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi kwa mwaka.
Kuratibu shughuli za huduma ya maji Wilayani.
Kusimamia ujenzi wa miundombinu na ukarabati wake Wilayani.
Kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji kwa maendeleo endelevu kwa kushirikiana na idara zingine.
Kuandaa taarifa na takwimu za huduma ya maji na kuziboresha kila wakati.
Mengineyo yanayojitokeza na kupangiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
MIKAKATI YA IDARA
Kuhakikisha huduma ya maji inaongezeka kutoka 44% iliyopo sasa mpaka kufikia 55 ifikapo Desemba, 2017.
Kuhakikisha miradi iliyopo inakuwa endelevu na inafanya kazi wakati wote.
Kuboresha taaluma ya watumishi ikiwa ni pamoja na maslahi yao.
Kuhakikisha Halmashauri inakuwa mstari wa mbele katika kuhudumia wananchi kwa ujumla
Takwimu za Maji Wilayani
Aina ya Teknolojia |
Iliyojengwa |
Inayofanya kazi |
Isiyofanya kazi |
Visima vyenye mfumo wa jua
|
6 |
5 |
1 |
Visima vyenye pump za mikono
|
123 |
82 |
41 |
Miradi ya Maji Mtiririko
|
7 |
6 |
1 |
Miradi ya Maji ya Kusukumwa na Mashine
|
3 |
2 |
1 |
Jumla
|
139 |
95 |
44 |
Programu ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira
Serikali inatekeleza Programu ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira. Programu hii inagharamiwa na Serikali pamoja na Wadau wa Maendeleo na inatekelezwa katika Wilaya zote nchini. Kwa Wilaya ya Uvinza vijiji 6 ndio vimeanza na vinaendelea na utekelezaji wa miradi ya Maji chini ya Programu hii ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira. Vijiji hivyo ni Uvinza, Nguruka, Ilagala, Kandaga, Rukoma na Kalya. Utekelezaji wa miradi hii umefikia hatua mbalimbali za ukamilishwaji.
Aidha miradi hii ikikamilika itawahudumia wananchi wapatao 110,770 na inategemewa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji hadi kufika asilimia 55. Mchanganuo wa miradi hiyo ni kama ulivyoonyeshwa hapa chini kwenye jedwali:-
Kijiji |
Idadi ya Walengwa |
Teknolojia |
Gharama ya ujenzi |
Maelezo |
Kandaga
|
12,107 |
Mradi wa kusukuma na mashine, magati 22
|
394,504,280 |
Ujenzi unaendelea
|
Rukoma
|
10,781 |
Mradi wa maji mserereko, magati 31
|
1,028,195,080 |
Ujenzi unaendelea
|
Nguruka
|
43,036 |
Mradi wa kusukuma na mashine, magati 55
|
2,873,196,856 |
Ujenzi unaendelea
|
Uvinza
|
9,346 |
Mradi wa maji mserereko, magati 26
|
1,713,969,015 |
Ujenzi unaendelea
|
Ilagala
|
25,799 |
Mradi wa kusukuma na mashine, magati 34
|
1,264,048,776 |
Uko hatua za mwisho
|
Kalya
|
9,701 |
Mradi wa maji mserereko, magati 28
|
777,777,343 |
Uko hatua za mwisho
|
Jumla
|
110,770 |
|
8,051,691,350 |
|
Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji Kalya ikiwa katika hatua za mwisho
Ujenzi wa tanki la 300m3 linalojengwa eneo la Nyangabo katika mradi wa Maji Nguruka
Shughuli ya umwagaji wa zege tanki la 500m3 katika mradi wa maji Nguruka ukiendelea
Shughuli ya umwagaji wa zege tanki la maji Nguruka ukiendelea
Ufungaji wa formwork katika tanki la 500m3 Nguruka
Tanki la 300m3 katika mradi wa maji Ilagala
Shughuli za ufungaji mabomba katika Mradi wa Maji kalya
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.