Idara ya Viwanda na Biashara –Halmashauri ya wilaya ya Uvinza imeendesha zoezi la utoaji elimu ya biashara na ulipaji kodi kwa wafanyabiashara.
Zoezi hili limefanyika katika kijiji cha Lukoma kata ya Igalula ikiwa ni utekelezaji wa makakati wa utoaji elimu ya usajili wa biashara na ulipaji kodi kwa maendeleo ya taifa, elimu hiyo imetolewa tarehe 22 September 2022.
Elimu hiyo imetolewa na Afisa Viwanda na Biashara Godfrey Balyorugulu amesema zoezi la elimu ya biashara na ulipaji kodi litakuwa endelevu na linategemewa kuongeza mapato ya halmashauri ili kongeza uboreshaji wa huduma za jamii ndani ya wilaya ya Uvinza.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.