Zoezi la ugawaji wa vitabu vya mtaala mpya linaendela katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza, ikiwa ni kutekeleza maagizo ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Zoezi hili limefanyika katika Ofisi za Idara ya Elimu Msingi iliyopo Lugufu hivi karibuni katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka katika shule zote za wilaya ya uvinza,
Naye Afisa Elimu taaluma msingi Wilaya ya Uvinza Bw. Simon Mahela Boneka amemshukuru Raisi Samia kwa jitihada anazozionesha kuhakikisha vitabu mashuleni vinapatikana hali inayopelekea ufaulu wa Watoto mashuleni kwa wilaya ya Uvinza kuongezeka
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita, ndani ya miaka miwili ya utawala wa Mama Samia Suluhu Hassani vitabu mashuleni vinapatikana kwa wanafunzi kujifunzia”. Amesema Bw. Mahela.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.