Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Uvinza Bw. Acland Kambili amewataka wakuu wa shule zenye Miradi kufuata taratibu za force account ili kutekeleza Miradi ya maendeleo, kuepusha kushindwa kukamilisha utekelezaji wa miradi.
Hayo ameyasema Bw. Acland alipokuwa akizungumza na walimu wakuu katika ukumbi wa Jengo la utawala Halmashauri ya Wilaya Uvinza tarehe 8/11/2023.
"Walimu wanapaswa kuandaa Mipango na kuwashirikisha walimu wenzake shuleni ili kukamilisha Miradi kwa wakati na kuondoa sintifaham kwa jamii husika, hivyo mnapaswa kubadilika katika usimamizi wa miradi ya maendeleo" alisema Bw. Acland.
Kwa niaba ya Afisa manunuzi Wilaya ya Uvinza Bi. Ester Gwiboha amesisitiza katika uteuzi wa Kamati ya ujenzi kuhakikisha ushirikishwaji wa jamii inayozunguka mradi na wataalamu wa ujenzi na manunuzi kwasababu nyaraka zinakuwa zinatakiwa kwa ufuatiliaji wa mradi.
Bi. Oliva Lukinja mwanasheria wa Halmashauri pia amesisitiza mikataba ya Mafundi iendane na wakati wa mradi kwa kuwa Miradi imecheleweshwa kukamilika kutokana na mikataba kuwa nje wa wakati.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.