Kaimu Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya Uvinza Bw. Acland Kambili amefanya kikao kazi na baadhi ya Walimu wakuu na wakuu wa vituo vya afya kwa lengo la kuwakumbusha majukum yao.
Katika kikao hicho Bw. Acland amesisitiza kusimamia miradi ya maendeleo kwa weledi kwani kumekuwa na ubadhilifu ukifanyika hali inayopelekea miradi isikamilike kwa wakati, hivyo amewahakikishia Walimu wakuu na wakuu wa vituo vya afya kuwa hayuko tayari kuangushwa kwa uzembe
"Ubabaishaji katika kusimamia miradi ni chanzo cha kutofanikisha ukamilishaji wa Miradi. Hivyo mradi ukikutwa na kasoro Mkuu wa shule au Mkuu wa kituo cha afya linakuwa ni jukumu lako kwa kulibeba" alisema Bw. Acland.
Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Bw. John Nyakiha amesisitiza kanuni za usimamizi wa miradi uimarishwe kwa kuwa kila shule wanajua majukum yao katika kutekeleza miradi
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.