Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Kigoma yamefanyika katika kijiji cha Kidahwe, mgeni rasmi akiwa mkuu wa mkoa wa kigoma Mh. Thobias Andengenye
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh.Thobias Andengenye ameagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuendeleza kutekeleza mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili wa watoto na wanawake (MTAKUWA) 2017/18 -2021 kwa kipindi hiki cha kusubiri kuhuisha mpango huu, hivyo ametaka kuendelea na mchakato wa mpango MTAKUWA kwasasabu ni njambo jema na endelevu kwani linaongeza ustaarabu katika jamii.
Mh. Andengenye ameongeza kwa kusema kuwa watu wote kuendelea kupinga vita vitendo vyote vya unyanyasaji kijinsia na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, aidha kwa kutoa hamasa kwa jamii kulenga kuhimiza usawa katika ushiriki wa wananchi katika masuala elimu,biashara, uzalishaji, siasa na fursa zingine zinazojitokeza.
vilevile amewataka wanawake kutumia fursa na elimu zinazojitokeza katika halmashauri illi kuweza kutumia asilimia 10 ya mapato kupata mikopo ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Pia Mh. Andengenye amewataka viongozi wanawake kutumia nafasi zao ilikutimiza wajibuwa kwa lengo kudhihirija uwezo usio na shaka.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.