Ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani Kigoma limeziduliwa na mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Antony Mwakisu amesema elimu ya ushirika itolewe kwa wananchi ili waweze kujua maana ya ushirika.
Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanal Mwakisu amesema elimu ya ushirika inahitajika kupelekwa kwa wananchi ili wajue nini tunafanya kwenye ushirika na maana ya ushirika, hayo yamezungumzwa katika uzinduzi wa Jukwaa la maendeleo kwenye ukumbi wa Bongwe sekondary uliopo mjini Kasulu mkoani Kigoma
Pia Kanal Mwakisu ameongelea suala la uelewa mdogo kwa wajumbe wabodi za ushirika na watendaji katika majukumu yao unaopelekea kushindwa kupata hati safi kwa vyama vya ushirika.
Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kigoma Bw.Robert Kitambo amewataka viongozi wa ushirika kusimama katika misingi uadilifu katika majukum ili kuweza kufika mbali na kujitathimini kwa shughuli walizozifanya zinatija kwa wanachama. Pia ameelekeza SACCOS kutoa taarifa za kazi na kukata leseni kwa maelekezo ya Bank kuu.
Katika picha ni bidhaa zinazopatikana kutoka kwa wakulima wa mazao mbalimbali kwenye vyama vya ushirika.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.