Ukuawaji wa tekinolojia umepelekea kwa Kampuni ya minara ya simu (HTT INFRANCO Ltd) kubomoa mnara Lugufu (eneo: Lugufu ID 4094) kutokana na changamoto za kimawasiliano kwenye mnara huo uliopo kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza hivi karibuni.
Kampuni hiyo imekusudia kubomoa Mnara Lugufu ID. 4094 na miundombinu yake imeshahamishiwa kwenye Lugufu KIG 009 ilikuweza kuthibiti uendeshaji wake kutoka na huduma kuwa hafifu uliotokana na changamoto za ukuwaji wa kitekinolojia kupishana na miundombinu iliyokuwepo hapo awali.
Mtaalam Emmamuel Mmasi kutoka kampuni ya minara ya simu amesema ni muda wowote kuanzia sasa zoezi la kuubomoa mnara linatarajia kuanza tayari kibari kutoka halmashauri ya wilaya ya Uvinza kimekamilika kuendelea na zoezi la ubomoaji.
Tatizo la mawasiliano katika halmashauri ya wilaya ya Uvinza bado ni changamoto kwa watumiaji hali inayopelekea kupata changamoto katika matumizi ya mawasiliano.
Naye mkuu wa kitengo cha TEHAMA halmashauri ya wilaya ya Uvinza Prudence Kalugira, ameyataka makampuni ya minara ya simu kuboresha mawasiliano kwani imekuwa kikwazo kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.