Pikipiki 6 zimetolewa kwa Watendaji Kata wa Halmashauri ya wilaya Uvinza katika adhima ya utekelezaji wa shughuli kwa urahisi.
Kwa awamu hii kata 6 zilizo na changamoto ya usafiri zimepata pikipiki katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika ngazi ya kata kwenye viwanja vya ofisi ya ardhi iliyopo halmashauri ya wilaya leo tarehe 6 machi 2023.
Akikabidhi pikipiki kwa watendaji wa kata 6, Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Uvinza Bw.Bernad Rusomyo amewataka kutunza na kuzilinda mali za serikali, amesema hatuna budi kuishukuru serikali ya mama samia suluhu hasani kwa kukabidhi vitendea kazi kwa ngazi za chini.
Bw. Bernad ameongeza kwa kusema pikipiki hizi vitumike kuimarisha utendaji kazi kwa kuwafikia wananchi na kuweza kutatua migogoro kwa moyo wa uzalendo ili kulinda tunu za Tanzania, kwa kuimarisha umoja na upendo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza Bw. Kechengwa Masumbuko amewakumbusha watendaji kata kuwa pikipiki hizi ni mali ya serikali, hivyo inapaswa kutunzwa sio tu kwasasabu unaweza kuhama ndio ukaharibu lahasha, hata ukihamishwa inabaki katani kwa matumizi ya kata pia amehimiza kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wilaya ya Uvinza, Bw. Acland Kambili amesema serikali imegawa pikipiki kwa watendaji kata nchi nzima, kwa wilaya ya Uvinza tumepata pikipiki 6 zitakwenda kufanya shughuli ngazi ya kata kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji ili kurahisisha usafiri wa kuwafikia wananchi katika maeneo yao. Hivyo amesema pikipiki zitumike kwa kutunzwa na sio kuweka ndani bali katika shughuli
OCD wa wilaya ya Uvinza afande Alfred amesema hata kama ni mtendaji kata au mtumishi yeyote, sheria ya usalama barabarani haikuondolei kinga ya kuvunja sheria. Akitoa elimu ya usalama barabarani amewataka watendaji kata wanaokabidhiwa pikipiki kuzingatia sheria za kanuni za usalama barabarani.
Kwa niaba ya Watendaji Kata Bi Zulfa ameishukuru serikali ya Raisi mama Samia Suluhu Hasani kwa kutambua ugumu wa kazi za watendaji kata kwa kusaidia kutoa pikipiki hizi kurahisisha utendaji kazi, hivyo amewaomba waliopata pikipiki kuzitunza na kuzithamini kama mali zao.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.