Maafisa Ugani wilaya ya Uvinza wamepata mgao wa pikipiki 16 kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wa shughuli za kukuza kilimo ikiwa ni Ajenda ya 10/30 Kilimo ni Biashara.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa maafisa Ugani na Afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Uvinza Bw. Bernad Rusomyo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Uvinza leo tarehe 6/03/2023 kwenye viwanja vya Ardhi.
kwa upande wake Afisa Kilimo wilaya ya Uvinza Bi.Toligwe K. Musongwe amesema ili afisa ugani aweze kutekeleza mkakati wa ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara ni lazima asimame katika nafasi yake. Hivyo amewataka maafisa hao kuchukuwa maamuzi sahihi yanayotolewa na serikal na kukifikisha kwa wakulima kwa usahihi.
Mmoja wa maafisa Ugani kwa niaba ya maafisa hao, amesema anaishukuru serikali kwa kuwagawia pikipiki ili kuweza kufika kwa urahisi mashambani kwa wakulima na kutatua changamoto wanazokutana nazo, na ameipongeza serikali kwa juhudi wanazo zionesha katika kuhakikisha kilimo inakuwa ili kuboresha uzalishaji kwa wakulima.
OCD wilaya ya Uvinza afande Alfred K.Mwalubilo ametoa elimu ya usalama barabarani kwa Maafisa Ugani kutumia pikipiki kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.