Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Mathamani ameahidi kutoa ushirikiano kwa shirika lisilokuwa la kiserikali TUUNGANE mara baada ya kupokea taarifa ya shughuli zao ndani ya halmashauri ya wilaya ya Uvinza.
Hayo Mh. Dinah ameyasema katika kikao cha TUUNGANE na timu ya watalam(CMT) kutoka katika halmashauri walipokutana kwenye ukumbi wa Jengo la Utawala katika hospitali ya wilaya ya Uvinza
Naye mkurugenzi wa mradi wa Tuungane Bw. Likindo A. Hiza amesema shirika hilo limefanya kikao na mkuu wa wilaya na timu ya wataalam wa halmashauri ili kukuza ushirikiano na kutambulisha shughuli mbalimbali wanazo tekeleza katika halimashauri ya Uvinza kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikumba halmashauri hususani katika kutetea haki za wanawake na kuweza kuwainua katika fursa mbalimbali.
Pia Bw. Hiza amesema ushirikiano huu utaboreshwa kwa mkakati walionao wakuanzisha utalii wa kutembelea Hifafdhi ya Mahali kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na timu ya wataalam wa halmashauri
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.