Mkutano wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) wa nusu mwaka wa wadau wa maji, wilayani Uvinza umefanyika tarehe 21 Novemba 2022 katika ukumbi wa vijana kata ya Kazuramimba.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbaimbali ngazi ya mkoa na wilaya kwa lengo lakutaka kusikiliza changamoto zinazoikabili miradi ya maji kwa wilaya ya uvinza ili wananchi waachane na adha ya maji.
Kaimu Mkuu wilaya ya Uvinza Bw. Liwaza Msasa ambaye ni Katibu Tarafa ya Ilagala amesema serikali inawahakikishia wanachi kupata maji safi na salama kwa kulinda miundo mbinu ya maji hivyo ameipongeza RUWASA na wadau wanaochangia miradi ya maji kwa wilaya ya Uvinza kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.
‘kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita Uvinza ilikuwa na changamoto ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali lakin kwa kiasi kikubwa, miradi hii imesaidia hata kupunguza umbali wa kuyapata maji, na serikali itaendelea kupeleka miradi ya maji pale ambapo haijafika,
Ameongeza kwa kusema kuwa serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kutekeleza miradi ya maji, hivyo amewaomba wadau wa maji na wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundo mbinu ya maji.
Pia Bw. Liwaza amevitaka vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) kutumia vizuri fedha wanazokusanya za uuzaji wa maji ili kuendeleza miradi ni pamoja na kusoma mapato na matumizi na sio kuzitumia hovyo kwa kujilipa posho hali itakayosababisha miradi kufa, ambayo itawarudisha wananchi kwenye shida za maji za wakati wa nyuma.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Uvinza Mh Jackson Mateso, akizungumza katika mkutano huo ametoa wito kwa wadau wamaji kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kulinda miundombinu ya miradi maji na kutoa taarifa pale wanapoona mabomba yamepasuka ili yafanyiwe matengenezo ya haraka ili wanachi wapate huduma.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wilaya Uvinza Mhandisi Jefta A.Julius amesema lengo la mkutano huo wa RUWASA na wadau wa maji ni kujadili utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa jukum la RUWASA kutekeleza miradi ya maji kwa wanachi na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta ya maji kwa kuboresha huduma ya maji.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.