Mkurugenzi Mkuu wa Multiplex Systems Limited Eng. Thomas Leopold Kalunga ametambulisha mradi wa kufua umeme kwa hatua za awali kutokana na maporomoko ya maji yaliyopo Kijiji cha Rukoma.
Hayo yamebainishwa na Eng. Thomas alipokuwa akiwajengea uwezo na uelewa wa mradi huo wakuu wa idara katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza kwenye ukumbi wa Jengo la utawala la Halmashauri leo tarehe 2 Novemba 2023.
Bw. Thomas amesema kutokana na fursa zilizopo Wilaya ya Uvinza ni jukumu la wawekezaji kuja kuwekeza, amependelea kata ya Igalula Wilayani Uvinza kutokana upatikanaji wa maporomoko yenye kina kirefu kwa ufuaji wa umeme ambayo watashirikiana na REA katika kuhakikisha umeme unapatikana .
Mradi unategemea kuzalisha jumla.ya megawati 5.34 za Umeme wa nguvu za maji katika maporomoko ya mto Luegere.
Mradi huu unaleta fursa kubwa za Umeme wa uhakika kwa shughuli mbali mbali za maendeleo na kuvutia uwekezaji mkubwa kama viwanda vya uzalishaji na kusindika bidhaa na kuongeza mnyororo wa thamani (value adding chain) katika Wilaya ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla.
Mradi huu ukianza rasmi utaleta ajira za moja kwa moja wa vijana na watoa huduma mbali mbali ikiwemo fursa za ukandarasi kwa wakazi wa Wilaya ya Uvinza
Kwa upande wake Bw. Kechegwa Masumbuko kwaniaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Uvinza amemtaka mwekezaji huyo kuwasilisha vielelezo vyote vya mradi ofisi ya Mkurugenzi kwa lengo la kujiridhisha kabla ya kupokea mradi huo rasmi kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Uvinza.
Pia Bw. Kechegwa ametoa angalizo la uwepo wa maji yatakayotosha kwa shughuli za umwagiliaji zinazofanyika Kijiji cha Rukoma kuchukua taadhari wa kukauka kwa maji.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.