KUKOSEKANA UMAKINI WA VYAMA VYA USHIRIKA
Kukosekana kwa umakini kwenye bodi za vyama vya ushirika kunapelekea vyama vyingi kushindwa kujiendeleza na kukua kutokana sintofahamu kwa baadhi ya wajumbe kujinufaisha wao hali inayopelekea vyama hivyo kufa na vingine kusindwa kutimiza malengo yao.
Mpaka sasa vyama vya msingi 7 kati ya 48 vinalegalega japo kuwa bado vinatambulika, lakini inafahamika kuwa sababu halisi ikiwa ni viongozi wa chama kuwa na tama ya kujilimbikizia majukumu yote ya chama cha msingi.
Hivyo Chama cha ushirika –Mwanyaka katika kijiji Mwamila kata ya Kazuramimba wamemvua ujumbe wa bodi Ally Bugelima kwa kukiuka taratibu na kanuni za chama cha msingi hali iliyopelekea wanachama katika mkutano mkuu kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye mjumbe huyo nakumtaka ajiudhuru ni katika ofisi ya mtendaji Mwamila tarehe 12/9/2022.
Naye Mwajuma Ally Mayunga mwanachama wa chama cha Mwanyika amesema wamezalisha bidhaa lakini bwana Ally Bugelima kwasababu ni wakala ameweza kuandika watu majina pembeni na kuwatafutia masoko wakati wanachama wake hawana pakupeleka bidhaa.
Uamuzi wa kumtoa mjumbe wa bodi umefanyika mbele ya afisa Ushirika Cathberth Dongwe baada ya kuwajengea uwezo wa kichama baada ya chama hicho cha msingi kukosa soko msumu huu wa mavuno kutoka na Ally mjumbe kuwa wakala wa pembejeo kutumia nafasi hiyo kudanganya wanachama wa Mwanyaka bei ya mazao na kutofikisha taasifa kwa usahihi na kuficha taarifa za kichama.
Pia Cathberth amesema ili kuimarisha chama umoja na ushirikiano ndio nguzo kubwa itakayopelekea kuleta ruzuku nyingi kutoka kwa wahisani kwani watakuwa wameona kile mlichokifanya.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.