Mafunzo ya Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa ya kuwajengea uwezo wakuu wa idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya Uvinza yamefanyika katika ukumbi wa Jengo la utawala Lugufu.
Mafunzo hayo yameendeshwa na Mratibu wa O& ODs Mkoa wa kigoma Bw. Erick Sanka amesema lengo la mafunzo ni kuwasaidia wakuu wa idara na vitengo kutekeleza majukumu yao kupitia mpango mkakati waliojiwekea kwa maendeleo ya Halmashauri.
Bw. Erick amesisitiza kuwa mafunzo haya yanasaidia kuchochea maendeleo endelevu kwa hi jamii, kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi katika uwazi na uwajibikaji na pia kuimarisha ushirikiano baina serikali na wananchi. Na ili kufikia malengo ya Mfumo huo, Fursa na Vikwazo vinapaswa kubadili mtazamo wa watu katika kuleta maendeleo kwa kutambua kuwa wao ni wadau wakuu wa maendeleo.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Mipango kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Uvinza.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.