UVINZA-KIGOMA.
SHIRIKA Lisilo la Kiserikali la NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY Linalotekeleza Mradi wa Masuala ya Haki za Binadamu, Afya, Elimu na Mazingira limeanza mpango wa kuwawezesha Vijana kutoka Kata zote za Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma katika masuala ya stadi za maisha kwa lengo la kuwa mabarozi katika maeneo ya Jamii.
Zaidi ya Vijana Arobaini kutoka katika kitongoji kimoja ndani ya kata moja, wamewezesha elimu ya stadi za maisha na watakuwa mabarozi kwa kuelimisha jamii katika masuala ya Afya, Mazingira na haki za binadamu wakianza na watoto walio katika umri wa miaka kumi na tatu hadi miaka kumi na saba.
Katibu Mkuu wa Shirika la NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY Staphodi Chamgeni amesema mpango ni kuwaanda vijana kwa kufanya utafiti kutoka katika maeneo yao, kwa lengo la kuwatambua mazingira yao ya kuishi na mienendo yao ya maisha, kwa lengo la kuwasilisha maoni katika mitaala itakayo wawezesha kutatua changamoto zinazowakabili.
“Alisema Vijana wengi wakekuwa na changamoto nyingi na hawajui pakuzifikisha na kupata utatuzi hivyo utafiti utabaini na kutatua kero zilizopo kwa vijana na kuwafanya kufikia ndoto zao na kuwa change katika kuchangia maendeleo yao na Taifa”
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Shirika la NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY Btrice Mtesigwa Amesema Mradi umeamua kulenga Vijana kwa kuwa wanaweza kurekebishika kitabia na kwamba, wataelimishwa masuala ya stadi za maisha ili kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi.
Bi. Mtesigwa aliongeza kuwa pamoja na juhudi hizo Vijana wengi wameporomoka Maadili hasa kuthamini wazazi, wazee na kwamba hatua hiyo imepelekea vijana kuingia katika matukio mengi ya uhalifu hivyo kutambua vijana kuanzia umri mdogo kutawezesha vijana kupata elimu na kutambua nini cha kufanya na kuwa na tabia njema.
“serikali ione nmna ya kushirikiana na wadau katika kuelimisha vijana kutambua nafasi zao na kuheshimu wazazi na wazee ili kujenga kizazi bora na chenye maadali bora katika jamii alisema”
Aidha baadhi ya Vijana waliowezeshwa elimu kwa kuwa mabarozi katika jamii katika kuelimisha vijana wengine akiwemo Hekima Barosha na Frola Amos wakazi wa Mji wa Nguruka Uvinza Kigoma, wameomba Serikali kuwapa nafasi vijana katika masuala ya Mikopo na stadi za maisha kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Walieleza kuwa, Vijana wengi wamehitimu vyuo nchini na kwamba wamebaki na elimu bila mafanikio, ambapo wamesema Vijana wengi wamejiingiza katika matukio mbalimbali ya kujihatarisha ili kupata vipato visivyo na haki na kwamba serikali kwa kufanya hivyo kutawezesha vijana wengi kujikwamua kiuchumi kupitia ajira ndogondogo watakazo anzisha.
Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Christopher Mtabazi amewataka vijana waliowezeshwa mafunzo ya kusaidia Vijana wengine kutekeleza maelekezo yote, bila kujali umbali ili kuchangia stadi za maisha kwa vijana wengi na mafanikio kupitia mradi huo.
Bwana Mtabazi aliongeza kuwa Vijana wanazo Frusa Nyingi Huku akiwasihi kuchangamkia mikopo inayotolewa na halmashauri ya alimia nne kwa vijana, ili kufanya kazi kwa bidii na kujipatia kipato na kuunga maendeleo ya Taifa.
“vinaja wengi wakiwemo wasomi wameshidwa kujiajiri na kusubiria ajira toka serikalini na kuwafanya vijana wengi kushidwa kutimiza ndoto zao, na wamekuwa tegemezi kwa wazazi licha ya kuwa chachu katika ukombozi wa familia zao”
Bwana Mtabazi aliongeza kuwa vijana wanatakiwa kuamka na kufanya kazi na kuepuka utegemezi kwa kufanya kazi, na kuwasihi kuunda vikundi vitakavyo wawezesha kupata mikopo serikalini na kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi, na kuendelea kushirikiana na mashirika mbalimbali kwa kupata elimu kama ambavyo shrike la NGURUKA DEVELOPMENT AGENCY linavyoendelea kuwezesha vijana kwa kuwapa elimu.
Mafunzo hayo yametolewa kwa siku tatu na vijan zaidi ya arobaini watakuwa mabarozi kwa jamii kwa kujua changamoto zinazo wakabili vijana walio katika umri wa miaka kumi na tatu na kumi na saba ili kuwajengea uwezo na kutatua changamoto zilizopo ndani yao kwa lengo la kufikia mafanikio na ndoto zao
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.