DC HANAFI: AMEONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA SENSA WILAYA YA UVINZA.
Mh. Hanafi Msabaha ameongoza kikao cha kamati ya Sensa ya watu na makazi agosti 2022 wilayani Uvinza kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi ili wajitokeze kushiriki kikamilifu.
Kikao hiki kimeudhuliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye ukumbi wa hospital ya wilaya ya Uvinza hivi karibuni.
Kamati ya Sensa ya watu na makazi imekutana kujadili utekelezaji wa sensa ya watu na makazi 2022. Katika kujadili utekelezaji wa sensa ya watu na makazi, kamati imepokea taarifa ya hali ya maandalizi katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23 agosti 2022.
Aidha Mh. Hanafi amesema kikao hiki kimekutanisha wanakamati ili kuonesha ushirikiano na ushirikishaji wa kujua nini kifanyike kwa muda huu ili utekelezaji ufanyike kwa kiwango cha juu kwani mwaka huu Sensa ni tofauti na miaka mingine.
Akitoa maelezo ya hali ya Sensa, Mratibu wa Sensa wilaya ya Uvinza Phaustin Temula amewataka wajumbe wa kamati hiyo kutoa elimu na kutoa hamasa mara kwa mara kwenye maeneo yao ya kazi za kila siku.
Wajumbe wa kamati ya Sensa ya watu na makazi wameahidi kutoa ushirikiano kwa makubaliano ya kufanya kazi hii kwa weledi na kwa kutumia nafasi zao kwa kutoa hamasa kwenye maeneo yao.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.