Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh.Dinah Mathamani amekabidhiwa jengo la mwaro wa kijiji cha Buhingu kutoka shirika la TUUNGANE kwa lengo la kuwasaidia wavuvi kuhifadhi mazao ya ziwani katika hali ya usalama.
Mh. Dinah amefurahishwa na kuishukuru TUUNGANE kwa ujenzi wa mradi huu kwani utasaidia kuhifadhi mazao ya samaki na kuweza kuyasafirisha mpaka nchi za nje zikiwa katika ubora wake, hayo ameyasema mbele ya wakazi wa kijiji cha Buhingu kata ya Buhingu.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.