Afisa Kilimo Bw. Frolian Cheusi amewataka wajasiliamali (walanguzi) kuacha tabia ya kutumia mabakuli ya lumbesa kwa wakulima wa Kijiji cha Basaza kata ya Basanza.
Hayo ameyasema Bw. Frolian mapema wiki hii, alipokuwa akizungumza na wakulima Pamoja na wajasiliamali baada ya kukusanya bakuli zinazotuka kupima lumbesa ikiwa mkulima anauza kilo moja kwa elfu mbili walanguzi wanapima elfu mbili hiyo kwa bakuli ambalo amelipunguza ukubwa ni mbinu ya kuwanyonya na kuwaumiza wakulima kwa maslahi yao binafsi.
Zoezi la kusanyaji wa bakuli za lumbesa limekuwa likitekelezwa na mtendaji wa Kijiji mara kwa mara katika siku za masoko ili kukomesha changamoto hiyo,na kuwapa elimu kwa lengo la kuwakumbusha umuhimu wa kufuata matakwa ya sheria ya vipimo kabla na baada ya msimu wa kilimo kuanza.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.