Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Uvinza Bi. Zainab.S.Mbunda akielezea mradi wa BOOST katika halmashauri namna ya utekelezaji wake mbele ya Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh Dinah Mathamani mara baada ya kupokea fedha zenye thamani ya bilioni 1.502,600,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika shule saba kwenye halmashauri.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Bi.Zainab katika ukumbi wa Afya Zamani uliopo halmashauri.
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Mathamani amesema fedha za mradi huu zifanye kazi kama ilivyokusudiwa, atamchukulia hatua za kinidham msimamizi yeyote atakaye onekana kukwamisha mradi.
"mradi huu unalengo la kuborsha miundombinu na sio vinginenevyo, nitamchukulia hatua za kiniidhamu msimamizi yeyote atakayeonekana kukwamisha shughuli za ujenzi huu katika shule zote" amesema Mh. Dinah
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.