Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya Uvinza wamepokea mradi wa kujenga ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima wadogo wadogo kwa njia ya KILIMO MSETO katika uzalishaji wa hewa ukaa utakaotekelezwa katika tarafa zote kutoka shirika la Rafiki wa Ziwa Tanganyika (FOLT).
Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa jengo la Utawala katika hospitali ya wilaya Uvinza.
Kwa niaba ya Meneja mradi wa Hewa Ukaaa, Bw. Kechegwa Masumbuko amewasilisha taarifa ya mradi huo kwenye baraza la madiwa kabla ya utekelezaji wa mradi kwenye tarafa husika. Mradi huu unatekelezwa na Friends of Lake Tanganyika (FOLT) kwa ufadhili wa Value Network Venture Advisory Services Pte.Ltd Company (VNV)
Katika hatua nyingine madiwani wameomba kamati zilizopangwa katika utekelezaji wa mradi zivunjwe ili kubaki na wataalam wachache watakao saidia kufanya kazi kwa haraka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mh.Jackson Mateso amewataka wataalam wa halmashauri kushirikiana na shirika la FOLT ili waweza kutekeleza mradi huo bila kuwa na usumbufu.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri Bi. Zainabu Mbunda ameshukuru shirika la FOLT kwa kuchagua wilaya ya Uvinza kutekeleza mradi huo kwani itasaidia kuongeza pato la halmashauri kupitia wananchi watakao fanya kilimo hicho.
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.