• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
UVINZA DISTRICT COUNCIL
UVINZA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Idara/Vitengo
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mpango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo yaJamii na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi na Zima Moto
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Mipango miji na mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Whe. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Livestock & Fishing

Idara ya Mifugo na Uvuvi

1.0     Utangulizi

Idara ya mifugo na uvuvi inaundwa na sekta mbili za mifugo na uvuvi. Idara inayojishughulisha na usimamizi wa wanyama wote wafugwao wakiwemo jamii za ndege pamoja na usimamizi wa shughuli za uvuvi na ufugaji samaki. Idara ina jumla ya vitengo 2, kitengo cha mifugo chenye watumishi 11 na kitengo cha Uvuvi chenye watumishi 8 (Me 7 na Ke 1)

2.0     Lengo la idara

Kusimamia maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi kwa kutoa elimu ya ufugaji na uvuvi endelevu kwa wadau wa sekta wilayani ili kuongeza tija, kuboresha hali ya uchumi na kuinua maisha ya wananchi kilishe na kimapato ili kuchangia pato la taifa. 

3.0     Majukumu ya Idara

Kutafsiri na kusimamia sera, sheria, miongozo na mikakati ya mifugo na uvuvi katika ngazi ya wilaya.

Kuratibu na kusimamia utendajikazi wa wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi wanaotoa huduma mbalimbali za maendeleo ya mifugo kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Kushirikiana na taasisi mbalimbali za utafiti ili kufanya utafiti wa mifugo, kupokea na kusambaza matumizi ya matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi.

Kushirikisha jamii katika kuandaa mpango wa maendeleo wilayani (DADP’s) kwa kuendana na mahitaji ya jamii katika wilaya.

Kusimamia na kuendeleza rasilimali zinazotumika kuendeleza ufugaji na uvuvi.

Kufanya tathimini mbalimbali za shughuli za mifugo na uvuvi, mahitaji na usambazaji pembejeo za mifugo

Kuratibu na kusimamia doria kudhibiti uvuvi haramu katika bwawa la Mtera

Kuelimisha wavuvi na jamii juu ya usimamizi shirikishi wa mialo (BMU’s), uvuvi haramu, leseni na usajili wa vyombo vya uvuvi pamoja na mazingira ya makazi ya samaki.

Kuendeleza ufugaji wa samaki katika mabwawa ya kuchimbwa kwa wakulima na wafugaji.

Kukusanya, kutunza na kutoa takwimu na taarifa sahihi za maendeleo ya mifugo na uvuvi wilayani

4.0     Vitengo vya Idara ya Mifugo na Uvuvi

Idara ya mifugo na Uvuvi ina vitengo saba ambavyo ni:

Kitengo cha Tiba na Kinga ya magonjwa ya Mifugo.

Kitengo cha Uendelezaji wa nyanda za malisho ya Mifugo.

Kitengo cha Uzalishaji Uboreshaji wa Mifugo na mazao yake.

Kitengo cha Utambuzi, Ufuatiliaji na Uandikishaji

Kitengo cha Udhibiti wa Ndorobo

Kitengo cha Uvuvi na leseni.

Kitengo cha ushauri na uelimishaji.

 

5.0     Fursa zilizopo

 

5.1     Mifugo 

  • Kuwepo maeneo ya malisho ya asili kwa kila Kijiji.
  • Maji ya kutosha  kutoka vyanzo  vya mito ya Malagarasi, Ruchugi, Rugufu,ziwa, nyamagoma,Sagara na Tangayika pia visima virefu.
  • Kuwepo raslimali mifugo na wafugaji.
  • Kuwepo miundo mbinu ya mifugo.
  • Kuwepo kwa wataalamu wa mifugo
  • Kuwepo kwa sheria, kanuni,sera na miongozo katika sekta ya mifugo
  • Kuwepo kwa fursa za masoko/minada ya mifugo.
  • Kuwepo wadau wa pembejeo za mifugo (wajasilia mali)
  • Kuwepo kwa eneo/ardhi ya wazi (General Land) inayofaa kwa ufugaji/malisho
  • Kuwepo kwa mazao yatokanayo na mifugo (nyama,maziwa, ngozi,mbolea ya samadi na mayai)

 

5.2     Uvuvi

1.  Kuwepo kwa Ziwa Tanganyika na maziwa madogo ya Sagara, Nyamagoma,

     Mto Malagarasi na Ardhioevu ya Malagarasi-Muyovosi (MMRS) na mito mingine

     mingi iayoingiza maji Ziwa Tanganika,Sagara na Nyamagoma.

2.  Kuwepo kwa aina nyingi za samaki (varieties of fish species). Kuna aina zipatazo

     300 katika Ziwa Tanganyika ikiwa ni pamoja na samaki wa mapambo

     wanaopatikana Ziwa Tanganyika (ornamental fishes).

3.  Kuwepo kwa rasilimali watu (Wavuvi).

4.  Kuwepo kwa wadau wa maendeleo katika sekta ya Uvuvi na Vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi.

5.  Kuwepo kwa maeneo yanayofaa kufugia samaki(Fish farming).

 

6.0     Idadi ya Mifugo

Halmashauri ina Ng’ombe wa asili wapatao 252,998, Ng’ombe wa maziwa ni 103, Mbuzi wa asili ni 198,240, Kuku wa asili 562,840, Nguruwe 135, Kondoo 40,450, Bata 20,534, Punda 230. Aidha, kuna  mbwa wapatao 6,829.

7.0     Eneo la Malisho

Halmashauri inakadiriwa kuwa na zaidi ya Ha. 200,000 zinazofaa kwa malisho lakini eneo linalotumika ni Ha. 67,304. Hii inamaanisha kwamba yapo maeneo yanayotumika kwa ufugaji ambayo si rasmi kwa ukilinganisha na takwimu za mifugo iliyopo hasa katika ardhi ya jumla ambayo inakisiwa kuwa na ukubwa wa zaidi ya hekta 120,000. Aidha jumla ya vijiji 59 katika mpango wa matumizi bora ya ardhi vimetenga maeneo ya malisho na katika vijiji hivi jumla ya Ha. 38,923.16 zimetengwa kwa ajili ya malisho.

Miundombinu 

Majosho 

Halmashauri ina majosho 15 kati ya hayo mazima ni 8 katika vijiji vya Uvinza 1, Uvinza ranch 7) na mabovu ni 7 katika vijiji vya Malagarasi 1, Mpeta 1, Lugufu 2, Itebula 1, Uvinza ranch 2).

Minada na banio

Halmashauri ina jumla ya minada 4 katika vijiji vya Chagu, Mpeta, Mwamila na Uvinza. Minada ya Uvinza na Chagu ina miundombinu iliyojengwa wakati minada ya Mpeta na Mwamila haina miundombinu.

Machinjio/Visahani

Halmashauri ina machinjio ndogo 3 zinazofanya kazi zilizopo Nguruka, Uvinza na Muyobozi.

Vituo vya Afya ya Mifugo

Halmashauri ina kituo 1 cha afya ya mifugo kilichoko Bweru – Itebula. Kituo hakifanyi kazi kutokana na kutokuwa na vitendea kazi.

Mialo

Halmashauri ina jumla ya mialo/maegesho ya uvuvi 16 ambayo hutumiwa na wavuvi. Kati ya mialo hiyo mwalo mmoja wa Muyobozi umejengewa miundombinu ya kissasa. Aidha, kuna maegezo rasmi 15 katika maeneo ya vijiji mbalimbali vya mwambao wa ziwa Tanganyika yanayosimamiwa na vikundi shirikishi vya rasilimali za uvuvi (BMUs).

Wilaya ya Uvinza ina jumla ya vikundi 16 vya ulinzi shirikishi za rasilimali za uvuvi katika vijiji 16 (Kalya, Sibwesa, Katumbi, Buhingu, Mgambo, Igalula, Rukoma, Kaparamsenga, Herembe, Tambusha, Kashagulu, Lufubu, Sigunga, Kirando, Karago na Muyobozi) mwambao wa Ziwa Tanganyika. Vikundi hivi vinakadiriwa kuwa na wanachama 2338.Vikundi hivi viliundwa kwa mujibu wa Sera ya Uvuvi 1997, Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za Mwaka 2009.

 

Kituo cha Doria Buhingu

Kutokana na harakati za makusudi za kudhibiti uvuvi haramu, mradi wa PRODAP umewezesha ujenzi wa kituo cha doria na usimamizi wa rasilimali za uvuvi ili kuwa na uvuvi endelevu katika kata ya Buhingu. Kwa sasa kituo hiki  kinafanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri pamoja na BMUs.

Nyumba za watumishi

10. Huduma muhimu zitolewazo mara kwa mara

Idara hutoa huduma mbalimbali za ushauri kwa wananchi kulingana na mkataba wa utoahji huduma kwa mteja na zaidi hujikita na masuala yafuatayo:

Ushauri juu ya uogeshaji mifugo

Huduma za chanjo ya kuku dhidi ya ugonjwa wa Kideri

Huduma na ushauri juu ya chanjo dhidi ya kichaa cha Mbwa

  • Matibabu dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo
  • Kutoa Elimu ya ufugaji bora
  • Kutoa kinga na matibabu dhidi ya minyoo
  • Kuhakikisha usalama wa nyama na walaji
  • Kutoa Elimu ya ufugaji bora wa samaki
  • Kutoa vibali vya uvuvi na ukusanyaji wa samaki

Matangazo

  • HER YA SIKUKUU YA SABASABA July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA SENSA July 18, 2022
  • TANGAZO WASIO NA NIDA July 19, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 25, 2022
  • Angaliza Zote

Taarifa za hivi Punde

  • Kilimo cha zao la PAMBA Uvinza

    March 22, 2023
  • Zoezi la ugawaji wa vitabu vya Mtaala Mpya -Uvinza

    March 16, 2023
  • Ukatili wa watoto ni urithi mbaya utatuangamiza na kututesa -RC Andengenye

    March 08, 2023
  • Serikali yakabidhi pikipiki 16 kwa Maafisa Ugani -Uvinza

    March 07, 2023
  • Angaliza Zote

Video

MAELEZO YA Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Uvinza na Mkurugenzi Mtengaji Kuelekea Nanenane 2020
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • News

Kurasa Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • Utumishi na Utawala Bora
  • TOVUTI YA MKOA WA KIGOMA
  • SALARY SLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Uvinza - Lugufu Area

    Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA

    Simu ya Mezani: 0282988503

    Simu: 0757894484

    Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.