Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko siku ya tarehe 24 March, 2018 alishiriki ujenzi wa Madarasa na Maabara katika shule ya sekondari Basanza, huu ni mwendelezo wa kushiriki pamoja na wananchi wa kata 9 zinazojengwa madarasa hayo ambazo ni Basanza, Mwakizega, Mganza, Kazuramimba, Mtegowanoti, Nguruka, Uvinza, Ilagala na Sunuka zilizopo wilaya ya Uvinza.
Katika juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madarasa zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi, jumla ya madarasa 44 na maabara 6 yanajengwa kwa nguvu za wananchi. Kazi hii ilianza Desemba 2017 hadi sasa madarasa 27 yapo hatua ya umaliziaji na 17 yapo hatua ya kufunga lenta.
Katika shule ya sekondari Basanza ambapo Mkuu wa wilaya alishirikiana na wananchi siku hiyo, uchimbaji wa msingi wa maabara 3 ulikamilika, pia matofari na mawe yalikusanywa eneo la ujenzi tayari kuanza kazi.
“Hakuna mtoto aliyefaulu darasa la saba atakayekosa nafasi ya kujiunga na kidatao cha kwanza” alisema Mkuu wa wilaya wakati akiongea na wananchi wa Basanza. Aliongeza kuwa tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo. Pia aliwapongeza wananchi wa Uvinza kwa namna wanavyojitolea kumaliza changamoto zao.
Mkuu wa wilaya alimalizia kwa kusema, “ Mgufuli hoyeeeeee”
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Uvinza Bw. Masumbuko Keche
akimtwisha tofali Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mrindiko
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe, Mwanamvua Mrindoko akishiriki kuchimba msingi.
Mhe. Mwanamvua Mrindoko mkuu wa wilaya ya Uvinza akizungu,za na wanachi wa kata ya Basanza
Uvinza - Lugufu Area
Sanduku la Posta: P.O Box 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0282988503
Simu: 0757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.