Leo tarehe 09/05/2019 hadi 11/05/2019 kutafanyika kongamano la wafanya biashara wa Nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika katika ukumbi wa NSSF Kigoma. Nchi hizo ni Rwanda, Burundi, Zambia, DRC Congo na Tanzania. Kongamano hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanual Maganga kwa kushirikiana na TCCI, TIC, KJP, AGRA, LIC, ITC na afropremere.
Mhe. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo. Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mrindoko kwa heshima anachukua nafasi hii kuwakaribisha Wafanya biashara wote katika wilaya ya Uvinza kushiriki Kongamano.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni:- "MIPAKA YETU KWA UCHUMI NA MAENDELEO"
UVINZA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la Posta: P. O. BOX 12 UVINZA
Simu ya Mezani: 0767355345
Simu: +255757894484
Barua Pepe: ded@uvinzadc.go.tz
Haki Miliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza . Haki zote zimehifadhiwa.