Wilaya ya Uvinza imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 397 na Tangazo la Serikali Na. 237 lililochapishwa kwenye gazeti la Serikali tarehe 09 Septemba, 2011. Halmashauri ya Wilaya ilianza tarehe 01 Julai, 2013. Halmashauri ya Wilaya Uvinza ilitokana na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.